Tuesday, April 13, 2010

NAS KUMLIPA KELIS DOLLA 10,000 KWA MWEZI...

Nas ametakiwa kumlipa mke wake wa zamani Kelis zaidi ya dola za kimarekani 250,000 kwa ajili ya matunzo ya mtoto wake na bili ya masuala ya kisheria katika kesi yao inayoendelea kuhusiana na suala zima la talaka
Jaji wa mahakama ya juu ya Los Angeles amemuagiza msanii nas kumlipa kelis dola 47, 249 kwa ajili ya matunzo ya mtoto pesa alizotumia mama huyo kumtunza mwanae na zaidi ya dola 155,787 kwa ajili ya bili ya kesi aliyofungua kwa ajili ya kudai talaka na hivyo Nas kutakiwa kulipa dola 10,000 kila mwezi na anatakiwa kulipa dola 48, 549.83 zilizotumika katika account ya kelis ambaye pia ni mwanamuziki na mbunifu wa mavazi
Wakati msanii huyo anakumbwa na maswahiba hayo lakini pia anatarajia kuja na album mpya ya Distant Relatives akiwa na mkali Damien Marley itakayotoka mei 18 mwaka huu, huku Kelis akitarajia kuja na album yake mpya iitwayo flesh tone ambayo itaanza kupatikana july 6

No comments: