Wednesday, December 16, 2009

JELA YA NUKIA KWA LIL WYNE 2010.


Rapa Lil Wayne ametokea mahakamani New York leo ambapo amepewa tarehe ya kutolewa kwa hukumu yake mwezi February mwaka 2010. Lil Wayne alikutwa na silaha mnamo October mwaka huu.
Rapa huyo, ambaye jina lake halisi ni Dwayne Carter, alitokea mahakamani hapo majira ya asubuhi, akisindikizwa na washkaji zake wa Cash Money Records, wakiongozwa na mkurugenzi wao Bryan “Birdman” Williams pamoja na Ronald “Slim” Williams
Lil Wayne alibaki kimya wakati jaji akitaja tarehe 9 February kuwa ni siku ya hukumu ya kesi inayomkabili, ambapo Wayne anaangalia kuchezea mwaka mzima nyuma ya nondo huko New York kwa kumiliki silaha kinyume na sheria.
Mwezi October, rapa huyo alikutwa na hatia hiyo ya kumiliki silaha kinyume na sheria. kesi hiyo inaibuka kutokana na kesi nyingine ya mwaka 2007 ambayo bunduki aina ya .40 calliber ilikutwa kwenye basi la Wayne analotumia kufanyia ziara sehemu mbalimbali.
Lil Wayne amezungumzia ishu hiyo hapo kwenye remix ya nyimbo ya “O Let’s Do It” aliyomshirikisha rapa Waka Flocka, ambayo baadhi ya mistari yake inasema:
Habari za hukumu hiyo ya Lil Wayne zimekuja wakati ngoma yake mpya aliyomshirikisha mkurugenzi wa Young Money Records na Eminem iitwayo "Drop The World" ikisumbua sana kwenye chati mbalimbali za internet.
Katika habari nyingine zinazomhusu Lil Wayne, uzinduzi wa albamu yake mpya ya Rebirth ambao ulitakiwa kufanyika baadae sana, umerudishwa nyuma hadi tarehe 1 February kutokana na kuwepo kwa hukumu hiyo.Albamu hiyo itaanza kuuzwa madukani siku chache baada ya Wayne kuanza kutumikia kifungo chake jela.

No comments: