Friday, March 12, 2010

AKON KUFANYA TRACK YA KIHINDI.

Nyota wa muziki wa R&B Akon anafuata nyayo za mwanamuziki Snoop Dogg kwa kurekodi track itakayotumika katika filamu huko Bollywood
Rapa Snoop alirekodi wimbo kwa ajili ya filamu ya kihindi ya Singh is Kinng ulikuwa mwaka 2008 lakini Akon anakuja na kazi katika filamu yenye jina la RA na ataimba kwa lugha ya kihindi na amefanya kazi hiyo bure
Nyota wa Bollywood Shah Rukh Khan ambaye ameonekana katika filamu hiyo amesema Akon ataonekana katika filamu hiyo licha ya kuimba na sasa amesafiri kuelekea Mumbai India akiwa na familia yake, marafiki zake na timu ya wanamuziki
Akon amesema India ni nchi ambayo amekuwa na ndoto ya kufanya kazi na anahitaji kufanya vitu tofauti na kufurahia kazi yake ambayo ataifanya kiasili na kwa kutumia lugha asiyoizoea".

No comments: