Thursday, March 18, 2010

CHAMILLIONAIRE"RAP SIO UHUNI.

Rapa kutoka kusini mwa nchi ya Marekani Chamillionaire ameelezea uwepo wa polisi wa hip-hop na kwa nini wasanii wanaorap wana tabia ya kuonyesha tabia za makosa ya jinai kupitia muziki. Chamillionaire amesema hivi sasa watu wengi wanashuhudia jinsi ambavyo wasanii wa rap wengi wanavyokwenda jela amesema ni tabia zao na si lifestyle ya muziki huu endapo mtu atakuwa akizungumzia masuala ya bunduki kila siku lazima maisha yake yatakuwa hivyo.
Naye produza wa kundi la Mobb Deep Alchemist naye pia amelizungumzia hilo na kusema marapa wanatofautiana na wengi huponzwa na marafiki mitaani, marafiki zao husababisha wajiingize katika biashara ya madawa ya kulevya wengine wakisikia VERSE zanazohusuyo bunduki hujua muziki wa rap unataka fujo jambo ambalo wanajidanganya na kusababisha hata polisi kujua kuwa marapa ni wahalifu

No comments: