Monday, March 8, 2010

KEYSHIA COLE KUPATA MTOTO WA KIUME.....

Msanii Keyshia Cole amebahatika kupata mtoto wa kwanza wa kiume aliyezaa na mchumba wake mchezaji nyota wa basketball Daniel Gibson anayeitwa Daniel Hiram Gibson Jr.


Keyshia Cole aliweka wazi tetesi kuwa ana ujauzito wa star huyo wa kikapu wa Cleveland Cavaliers mwezi January mwaka huu na kuahidi kuwa wanatarajia kufunga ndoa baada ya kuvishana pete ya uchumba katika mkesha wa mwaka mpya na mchumba wake huyo.

Taarifa ya kujifungua Keyshia Cole inakuja baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini siku chache zilizopita baada ya kudhaniwa kuwa siku zake za kujifungua zimefika lakini mambo yalikuwa bado labda ulikuwa uoga flani kwa mtoto wa kwanza.

No comments: