Wednesday, March 24, 2010

FAMILIA YAKINA BEYONCE YAONGEZEKA...

Familia ya waimbaji Solange na Beyonce ikiwa chini ya mzee Mathew Knowles hivi sasa wameongezeka baada ya baba yao kupata mtoto mwingine wa kiume baada ya kufanyika vipimo vya DNA na kugundulika kuwa Nixon ambaye ni mtoto wa kiume aliyezaliwa na mama Alexsandra Wright aliyedai kuwa na mahusiano ya mzee Knowles kwa zaidi ya miezi 18 ni mtoto halisi wa baba yake beyonce
Oktoba mwaka jana mwanamama Wright alifungua kesi mahakamani na mzee akatakiwa kutoa dola 8,200 kila mwezi kwa ajili ya kumhudumia mtoto huyo hadi pale mambo yatakapowekwa hadhharani baada ya vipimo vya DNA kufanyika
Kutokana na tukio hilo January mwaka 2009 mama mzazi wa Beyoncé Tina Knowles alifungua kesi mahakamani akitaka talaka kutoka kwa mumewe huyo waliyeishi pamoja kwa zaidi ya miaka 30 na kufanikiwa kupata watoto wawili Beyonce aliye na miaka 28 na solange aliye na miaka 23

No comments: