Friday, March 19, 2010

P DIDDY ANATAKA KUWA KAMA ABROMAVIC...

Sean “Diddy” Combs hivi sasa ana nia ya kuwekeza katika michezo hususani soka kwa kutaka kuinunuaclub ya soka ya Crystal Palace.Kwa mujibu wa Diddy anataka kujaribu kupata fursa hiyo ya kuinunua timu hiyo iliyo kusini mwa jiji la London kwa dau la paundi milioni 360 baada ya timu hiyo kufilisika mwaka huu mwezi january
Wakilithibitisha hilo wawakilishi wa rapper huyo wamesema ameangalia timu mbalimbali ili aweze kuzinunua lakini amevutiwa na Crystal Palace kutokana na jina lake hivyo ataungana na msanii mkongwe katika miondoko ya Hiphop Jayz ambaye anaendelea kujaribu kusaka soko la timu huko Ulaya
Ikumbukwe kuwa mwaka 2005 Jay-Z aliangalia uwezekano wa kuinunua Arsenal au timu ya Chelsea .Na endapo wazo la Diddy litafanikiwa basi atakuwa mkongwe wa kwanza wa hiphop kutoka Marekani kuwa mmiliki wa timu huko Ulaya

No comments: