Tuesday, March 16, 2010

JUSTIN BIEBER NYOTA YAZIDI KUNG"ARA.

Wasichana wengi wanaguswa na msanii Bieber, wasichana wengi waigizaji ni mashabiki wakubwa wa mkali Bieber na mara nyingi wamekuwa wakimwalika katika show zao zaidi ya mara moja
Kwa mara ya kwanza katika historia ya program ya ABC katika kipindi cha miaka 13 msanii huyo ataonekana mara mbili katika kipindi jumatatu ijayo na jumanne akitarajiwa kuungana na Barbara Walters, Whoopi Goldberg, Elisabeth Hasselbeck na Sherri Shepherd kwa mahojiano maalum na kufanya tamasha
Mkali huyo kutoka Canada atakamua kazi yake ya “Never Let You Go” na kazi yake iliyoshika namba moja kati ya nyimbo 20 katika chati ya Baby .
Bado hazijafika hatawiki sita tangu mkali Justin Bieber aingie Islam Def jam na kuja na album yake ya My World na baada ya hapo akaimba kwa ajili ya Rais . Obama katika tamasha maalum la “We Are the World,” na kuwagusa wakali Rihana naBeyoncĂ©.

No comments: