Rashid "snake boy" Matumla kuzichapa dec 6 mjini Iringa na Chupak chipindi katika show kubwa 'MTIKISIKO 2009'pamoja na kuwepo na burudani ya muziki kutoka kwa artist kibao lakini piiiiia Ebony int mwaka huu wakipewa sapport kubwa na VODACOM wameona sio kesi kudrop pambano la ndonga siku hiyo..Aaaaaaaah wametisha..
4 comments:
Asilojua Matumla ni kiasi gani anahatarisha maisha yake kwa kuendelea kupigana. Matumla hakutumia vema wakati wake alipokuwa kwenye chat. Angeweza kuwekeza na kutopigana ili "kuiona kesho". Na kama angewekeza wakati ule, basi sasa hivi angeenda kusomea ukocha akawa mkufunzi ama asomee uandishi ili awe boxing analyst wa kituo kimojawapo.
Lakini ndio hivyo tena. Too little too late na sasa atapigana kwa discount price mpaka mwisho wa maisha yake.
Nadhani angefanya mpango akapigane kwenye pambano la utangulizi la "mfulia" mwenzake Evander huko UG.
Blessings
Mimi nilitaka kuuliza. Naona hapo ana mikanda kibao - ni mikanda ya kimataifa au ya uchochoroni? Na kama alivyogusia Mzee wa Changamoto hapo juu - huyu jamaa nilimsikia zamani kidogo na nashangaa kwamba bado anapigana. Ni kwa sababu ya njaa au?
Ni hatari sana kuendelea kupigana hasa baada ya kufikisha miaka 40. Amuulize "The Greatest" atamwambia.
Ni kweli sasa hivi Matumla umri umekwenda,halafu na yeye mwenyewe ana kitambi sasa hivi ndio maana mzito akiwa ulingoni
Hahahaha Matondo.
Sina kumbukumbu ya rekodi yake kwa sasa lakini alijaribu kimataifa japo lishe na mazingira vilimuumiza. Nilienda kumhoji nilipokuwa Times Fm (sikumkuta nyumbani kwake) lakini mazingira anayoishi na hali ya nyumbani kwake unaweza kujiuliza kama anaweza ku-concentrate kwenye mazoezi.
Huyu alikuwa na kipaji japo hakuna aliyeweza kuking'arisha na matokeo yake ndio kwenda kuumbuka kama Tyson na sasa naona Evander anaweza kuwa next online.
Matumla anaonekana kavimba kabla hata hajaingia ulinoni, sasa sijui itakuwaje?
Lakini bado anastahili kuwa kwenye HALL OF FAMER YA BOXING nyumbani
Bless I 'n I
Post a Comment